Proverbs 3:13-18


13 aHeri mtu yule aonaye hekima,
mtu yule apataye ufahamu,
14 bkwa maana hekima ana faida kuliko fedha
na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.
15 cHekima ana thamani kuliko marijani;
hakuna chochote unachokitamani
kinachoweza kulinganishwa naye.
16 dMaisha marefu yako katika mkono wake wa kuume;
katika mkono wake wa kushoto
kuna utajiri na heshima.
17 eNjia zake zinapendeza,
mapito yake yote ni amani.
18 fYeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia;
wale wamshikao watabarikiwa.
Copyright information for SwhNEN